16 Septemba 2025 - 16:57
Mkusanyiko wa watu wa Venezuela katika kuunga mkono malengo ya Palestina na kulaani mauaji ya kimbari yanayoendelea Gaza

Katika jimbo la Vargas, Venezuela, vikundi na mashirika ya kijamii, kwa msaada wa "Jukwaa la Mshikamano na Malengo ya Palestina", siku ya Jumamosi tarehe 13 Septemba 2025, walikusanyika pamoja ili: Kulaani mauaji ya kimbari yanayoendelea Gaza, Kuonesha upinzani wao dhidi ya sera na vitisho vya serikali ya Marekani dhidi ya nchi yao, Na kusisitiza juu ya haki ya Venezuela ya kujitawala kama taifa.

Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (as) -ABNA-: Mkusanyiko huo ulifanyika kwa ushiriki wa idadi ya watu wa Venezuela, ambapo washiriki walionyesha mshikamano wao na watu wa Palestina kwa kushikilia mabango na kutoa hotuba mbalimbali za kuisapoti Gaza na Palestina kwa ujumla.

Wandau wa mkutano huo walilaani vikali mauaji ya halaiki yanayoendelea Palestina, na kwa nguvu walipinga sera na vitisho vya serikali ya Donald Trump kuhusu uwezekano wa kuingilia siasa za Venezuela.

Mkusanyiko wa watu wa Venezuela katika kuunga mkono malengo ya Palestina na kulaani mauaji ya kimbari yanayoendelea Gaza

Washiriki walisisitiza kuwa maandamano na shughuli za uungaji mkono wa watu wa Palestina yataendelea mitaani, na wakabainisha thamani za kibinadamu pamoja na mshikamano wa wananchi wa Venezuela.

Tukio hili ni sehemu ya jitihada za kudumu za watu wa Venezuela kuongeza uelewa juu ya hali mbaya ya Gaza na kulinda haki za mataifa pamoja na uhuru wa taifa lao.

Mkusanyiko wa watu wa Venezuela katika kuunga mkono malengo ya Palestina na kulaani mauaji ya kimbari yanayoendelea Gaza

Mkusanyiko wa watu wa Venezuela katika kuunga mkono malengo ya Palestina na kulaani mauaji ya kimbari yanayoendelea Gaza

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha